
Vidonda vya tumbo ni matokeo ya kuharibika kwa uteute wa ndani ya ukuta wa tumbo la Chakula au ndani ya utumbo mdogo wa Chakula, na matokeo yake ni ukuta wa tumbo kugusana na tindikali iliyoko tumboni ambayo ni kali sana kama maji ya betri.
- Vidonda vya tumbo husababishwa na maambukizi ya bacteria waitwao *HELICOBACTER PYLORI*, aidha matumizi ya baadhi ya dawa za kutuliza maumivu za jamii ya Non_steroids anti inflammatory drugs kama vile ASPIRIN /DICLOFENAC huweza kusababisha uwezekano wa kupata ugonjwa huu.
- Vidonda vya tumbo vinaweza kujitokeza katika utumbo mdogo na katika tumbo la Chakula na pia ni Mara chache huweza kujitokeza katika koo la Chakula ambapo hapakukusudiwa kustahimili tindikali ya tumbo.
*AINA ZA VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCERS DISEASE)*
Kuna aina nyingi za vidonda vya tumbo ambavyo ni
(a) Vidonda vinavyotokea katika mfumo wa Chakula yani tumboni.
(b) Vidonda vinavyotokea katika utumbo mdogo.
(c) Vidonda vinavyotokea katika koo /koromeo la Chakula.
*HATUA KUU ZA VIDONDA VYA TUMBO*
Ni vizuri kufaham kwamba huu ugonjwa una hatua nne ambazo ni muhimu
HATUA YA KWANZA ~ Uvimbe sugu unaotokea sehem ya ndan ya tumbo.
HATUA YA PILI
~ Vijidonda kujitokeza sehemu zenye uvimbe na taratibu vidonda hivyo huongezeka na kuwa vikubwa, katika hatua hii mgonjwa hupatwa na maumivu makali ya tumbo yanayodumu kwa muda mrefu yakiambatana na kiungulia, tumbo kujaa gesi wakati wote, kukosa hamu ya kula, choo kuwa kigumu au kukosa choo kwa muda mrefu, hata hivyo Hali hii ya kukosa choo kwa muda mrefu *(CHRONIC DYSPEPSIA)* yaani kushindwa kufanya Kazi kwa mfumo wa mmeng'enyo wa Chakula kutokana na tindikali nyingi inayozalishwa tumboni kuingia Kwenye mzunguko wa damu hivyo mgonjwa hujisikia uchovu na kizunguzungu cha Mara kwa Mara katika hatua hii tindikali husababisha magonjwa ya ini na Figo kwa kuwa tayar iko katika mfumo mzima wa damu.
HATUA YA TATU
~ Hii ni hatua ambayo ni ya hatari kwasababu vidonda vikubwa hupasua mishipa yote midogomidogo ya damu na kusababisha damu kuvia tumbon na kubadilisha rangi ya choo kuwa sio ya kawaida, pia damu nyingi ikivujia tumboni mgonjwa hutapika na kuharisha damu Hali hii husababisha mgonjwa kuishiwa damu Mara kwa Mara, maumivu makali ya tumbo,hupata Homa, maumivu ya viungo na kukosa hamu ya kula.
HATUA YA NNE
~ Katika hatua hii saratani ya utumbo inahusika kwani hatua hii vidonda vya tumbo hutengeneza tundu katika tumbo au utumbo mdogo na kusababisha kuoza kwa viungo vya ndani na matokeo yake ni saratani ya utumbo mpana.
*VISABABISHI/VIHATARISHI VYA VIDONDA VYA TUMBO*
Visababishi vya ugonjwa huu vipo vingi sana hivyo yatupasa kuviepuka ili kujiepusha na huu ugonjwa.
Zifuatazo ni sababu za ugonjwa huu
i. Utumiaji wa madawa ya kuondoa maumivu kwa muda mrefu.
ii. Mawazo na huzuni kwa muda mrefu.
iii. Kutokuwa na muda maalum wa kula.
iv. Utumiaji wa pombe.
v. Utumiaji wa madawa ya kulevya nk.
*DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO*
~Dalili za vidonda vya tumbo ni nyingi lakini sio watu wote wanaopata Dalili hizi Wana vidonda vya tumbo;
i. Maumivu makali au kiungulia maeneo ya chembe moyo *(EPIGASTIC PAINS)*
ii. Kuvimbiwa au tumbo kujaa gesi hali hii huweza kuendana na kucheua na kujamba Mara kwa Mara.
ii. Kutapika damu
iii. Mtu mwenye vidonda vya tumbo (gastric ULCERS) hupata maumivu makali pindi anapokula au amalizapo kula.
iv. Mtu mwenye vidonda vya tumbo katika utumbo mdogo (duodenal ulcers) hupata maumivu makali pindi anapokua na njaa.
v. Kupoteza hamu ya kula.
vi. Kupata choo kubwa yenye rangi damu na yenye harufu mbaya.
vii. Kupungua uzito.
Nina matumaini mpaka hapo kila mtu amenielewa na kama umenifuatilia kwa makini basi hujatoka bure na utakuwa umeelewa kuhusu vidonda vya tumbo na hatua 4 pamoja na aina ya vidonda vya tumbo na nini kisababishi.
Sasa hebu tuangalie nini unatakiwa kufanya kama una vidonda vya tumbo.
*MAMBO YA KUFANYA KWA MWENYE VIDONDA VYA TUMBO*
i. Epuka kula vyakula vyenye viungo vingi kama vile pilau.
ii. Epuka kutumia pombe.
iii. Epuka ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi.
iv. Kula Chakula kidogo kwa muda maalum.
v. Kula vyakula vyenye fiber yaani vyakula vyenye nyuzunyuzi ambavyo ni jamii ya mbogamboga na matunda.
vi. Epuka unywaji wa kahawa au kinywaji chochote chenye caffeine kiepuke.
Bila shaka mpaka sasa unajiuliza,
*"Nitafanyaje kama nina vidonda vya tumbo?"*
Napenda nikwambie kuwa matibabu ya ugonjwa huu yanapatikana vizuri nchini mwetu ila tatizo ni tiba yenyewe kutokua na wataalamu wa kutosha wa kutibu chanzo cha tatizo na kumaliza tatizo pasipo kuleta matatizo mengine.
Kutokana na matibabu yenyewe kuhusisha mfumo wa dawa za kemikali ambazo zina madhara kwa mhusika pia.
Hivyo tiba bora kwa vidonda vya tumbo ni mlo kamili na dawa zisizo na kemikali, pia tunapaswa kuepuka baadhi ya vyakula na kuzingatia masharti.
Mpaka hapo sina la ziada ahsanteni kwa wote mliofuatilia darasa hili.
Au Kama Kuna watu unaowajua Wana madonda ya tumbo tuwasiliane In-box kwa 0713417921
Offered By: Juma Simba *Not Blaqsbi*
Price: 50,000
In Stock: 1
Purchase Minimum: 1
Purchase Maximum: 1
Type: Health & Beauty
All prices exclude shipping costs
Available shipping methods: USPS Delivery 9,750